Inatafuta bidhaa za Majengo...
Uza | Nunua | Pangisha | Panga kwa urahisi
Ahsante kwa kuchagua G-Konekti.
Uza | Nunua | Pangisha | Panga kwa urahisi
Ahsante kwa kuchagua G-Konekti.
Tunakusanya taarifa mbalimbali za mtumiaji wa G-Konekti ili kuendelea kutoa na kuboresha huduma zetu; taarifa hizo zinajumuisha taarifa binafsi za mtumiaji (Jina, email, namba ya simu, jinsia na anuani ya makazi) Pamoja na taarifa nyingine ambazo zinaweza kuhusiana na taarifa tajwa kutoka kwenye washirika mbalimbali wa mtandao huu kama vile mitandao ya simu (Mobile Network Operators) ili kuongeza ufanisi wa utendaji kazi na utoaji wa huduma.
Kidakuzi/kuki ni faili dogo la herufi na nambari ambalo linatusaidia kukusanya taarifa zinazotumika kutofautisha baina ya mtumiaji/mtembeleaji mmoja wa G-Konekti na mwingine. Taarifa hizi muda mwingine huhitaji ruhusa ya mtumiaji ili kukusanywa. Vidakuzi husaidia kuboresha utaratibu na uzoefu wa kuvinjari katika mtandao, pia husaidia kuhesabu na kupata idadi ya watembeleaji na watumiaji wa mfumo (hata wasiokuwa na akaunti rasmi).
Taarifa zote zinazokusanywa na G-Konekti zimelenga matakwa na mahitaji rasmi ya kumudu utoaji huduma pamoja na taarifa za msingi zinazohitajika na G-Konekti. Hivyo, taarifa zote zinabaki kuwa mali ya G-Konekti na mtumiaji wa mtandao pekee na hazitatolewa mahali popote isipokuwa pale inapokubliwa na mmiliki wa taarifa.
G-Konekti inaweza kutoa baadhi ya taarifa za mtumiaji wa mtandao wa G-Konekti kama vile namba ya simu na jina la mtumiaji katika mazingira yafuatayo:
A. Mtumiaji wa mtandao (mteja) anapohitaji kununua bidhaa iliyotangazwa kupitia G-Konekti (Mteja atapatiwa namba ya simu pekee ya muuzaji wa bidhaa husika baada ya kutuma ujumbe wa awali kupitia utaratibu rasmi wa mtandao huu.
B. Mtumiaji wa mtandao (mteja) anapotuma ujumbe wa kuhitaji bidhaa/huduma iliyotangazwa kupitia G-Konekti (Muuzaji atatumiwa jina pamoja na namba ya simu ya mnunuzi ili kukidhi matakwa ya mawasiliano ya kibiashara baina ya muuzaji na mnunuzi).